Kumbukumbu za biashara ni muhimu sana hata ukizingatia msemo wa wahenga
kuwa mali bila daftari hupotea bila taarifa. Hivyo biashara bila
kumbukumbu ni sawa na bure. Kumbukumbu zina umuhimu na fadia zake ni
kama zifuatazo;
Mmiliki kujua faida halisi ya biashara
Faida
ya biashara inatokana na mapato baada ya kutoa matumizi, hivyo ni
dhahili ili kupata faida halisi mfanyabiashara anapaswa kuweka taarifa
zake za mapato na matumizi kwa usahihi na kweli.
Kulipi kodi
halali
Kipengele 80 cha sheria ya kodi ya mapato kinatoa nafuu kwa
mlipa kodi anayetunza kumbukumbu zake za biashara. Mfanyabiashara
asiyekuwa na kumbukumbu za biashara yake anaweza kudaiwa kodi kubwa
kuliko stahili yako. Hivyo kumbukumbu za biashara zinasaidia kulipa kodi
stahiki na sahihi.
Husaidia kufuatilia mtiririko wa biashara na
mapato
Mtiririko wa biashara unahusisha mambo mengi ikiwemo ununuzi
wa bidhaa, gharama za biashara, mauzo, wadeni na wadai na hata mali za
biashara. Kwa hiyo, kwa mfanyabiashara kuweka kumbukumbu za biashara
zitakuwezesha kujua hali na thamani ya mali, madeni na mtaji wa
biashara. Hali kadhalika, mtiririko wa fedha. Kwa ujumla utajua thamani
ya biashara yako.
Husaidia kuthibitisha au kutoa ushuhuda wa
miamala ya biashara
Mwendelezo wa utunzaji kumbukumbu za biashara
hufikia hatua ya kufanya ukaguzi wa mahesabu ambapo wakaguzi wa mahesabu
hukagua taarifa hizo ili kutoa ripoti ya taarifa za fedha. Nyaraka
zilizotunzwa vizuri mfano, stakabadhi, vocha za malipo na risiti zake
ndizo zitathibitisha kuwa kweli muamala ulifanyika na malipo au maingizo
ni sahihi.
Mamlaka ya Kodi nchini – TRA na hata benki huhitaji kuona
nyaraka hizo hizo za biashara ili kujiridhisha wakati wa kukadiria kodi
ya biashara yako hiyo.
Mahitaji ya wawekezaji
Wakati mwingine
unaweza kuhitaji kuongeza nguvu/mtaji wa biashara kwa kupitia njia ya
kutafuta mwekezaji au mbia, hivyo kumbukumbu ulizonazo ndizo
zitakazomfanya mwekezaji au mbia kutoa maamuzi. Na wakati mwingine
unaweza kutaka kuuza biashara yako, ili kujua bei au thamani ya biashara
hiyo kumbukumbu lazima ziwe zimetunzwa vizuri.
Kuongeza mtaji
kupitia mikopo
Watu wengi hutumia njia ya mikopo toka benki au
taasisi za fedha kuongeza mtaji wa biashara. Kamwe huwezi hata kusogelea
taasisi hizo kama huna kumbukumbu za biashara yako. Ili utembee kifua
mbele au taasisi za fedha zikufuate zenyewe kukuomba ukope kwao, ni
vyema utunze vizuri kumbukumbu za biashara yako.
Aina ya
kumbukumbu za biashara
Cash book – hurekodi taarifa zinazohusiana na
fedha taslimu au fedha iliyo benki kuingia (kupokea) au kutoka(kulipa)
MFANO
WA CHATI YA CASH BOOK
MWEKE
MTOE
Tarehe Maelezo
Taslimu Benki Tarehe Maelezo Taslimu Benki
2.4.11
Mauzo 20,000 2.4.11 Umeme 3,000
2.4.11
John kulipa deni 7,000 2.4.11 Usafiri 2,000
2.4.11 Taslimu 20,000 2.4.11 Kulipa kodi-TRA
1,500
2.4.11 Benki 20,000
Jumla 27,000 20,000 Jumla 25,000 1,500
Salio fungia 2,000 18,500
5.4.11 Salio anzia 2,000 18,500
Chati ya Cash Book ina sehemu kuu mbili yaani mweke na
mtoe. Mweke ni sehemu ambayo maangizo yote ya fedha taslimu na benki
huandikwa. Mtoe ni sehemu ambayo malipo au fedha iliyotoka huandikwa.
Hali kadhalika, kama fedha taslimu imepelekwa benki ni lazima pande zote
mbili ziandikwe, upande wa mweke na mtoe.
Mwisho wa kila siku
lazima ufunge kitabu chako kwa kupata jumla ya taslimu na benki upande
wa mweke na jumla ya taslimu na benki upande wa mtoe. Kisha kupata
balansi fungia kwa kuchukua jumla ya upande wa mweke kutoa jumla ya
upande wa mtoe. Salio fungia huandikwa upande wa mweke. Na mwisho
unafungua mstari wa chini ili kurekodi miamala ya siku inayofuata,
chukua salio fungia kuwa salio anzia, kisha mtiririko unaendelea(kama
hapo juu).
Petty cash – hurekodi matumizi madogo madogo ya fedha
taslimu katika uendeshaji wa kila siku wa biashara.
Debit and Credit
note – hurekodi taarifa zisizohusu fedha taslimu. Debit note hutumika
kuandika taarifa ambazo unategemea kupokea fedha (mali) na Credit note
hutumika kuandika taarifa ambazo unategemea kulipa fedha (deni).
VAT
Account – kwa biashara za kuuza bidhaa huwa zinakuwa na namba ya
usajili ya ongezeko la kodi - VRN, hivyo lazima uwe na akaunti maalum
kwa ajili ya kodi za VAT.
Purchase day book – hurekodi taarifa za
manunuzi ya bidhaa au malighafi kila siku.
Sales day book – hurekodi
taarifa za mauzo
Production records – hurekodi taarifa za
uzalishaji wa kila siku kwa wenye biashara za viwanda.
Bank statement
– hii ni taarifa kutoka benki inayoonesha mtiririko wa miamala ya
biashara yako kwa fedha zinazotoka au kuingia kwenye akaunti hiyo. Pia
hurekodi makato mbalimbali kama gharama za benki. Ni lazima kila
biashara kuchukua taarifa hii toka benki walau mara moja kila mwezi.
Mikataba
– biashara nyingi huwa zina mikataba mfano pango, kuleta bidhaa au
kuuza bidhaa au huduma. Mikataba hii ni muhimu sana kuwa kumbukumbu za
biashara.
Rekodi za kompyuta – biashara zingine hutumia mfumo wa
komputa hasa kupunguza kazi za makaratasi. Pia ni muhimu kuhakikisha
taarifa zinaingizwa vizuri na kutunzwa sehemu mbalimbali (back up).
Inashauriwa
ili uwe na kumbukumbu sahihi ni bora kuhakikisha fedha yote inaingia
kwenye akaunti ya benki na matumizi yote hutoka kwenye akaunti ya benki.
Hii itasaidi kudhibiti matumizi na kuleta nidhamu ya fedha.
No comments:
Post a Comment