Sunday, October 21, 2012

Maonyesho Ya Wajasiriamali Wanawake Dar


Mh. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Sophia Simba akishangazwa kwa umahiri na uzuri wa kazi za ubunifu za mmoja kati ya wajasiriamali wanawake walioshiriki Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Tanzania- TWENDE, 2011 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es slaam. Pembeni yake kulia ni Mh. Jerry Silaa, meya wa Halmashauri wa wilaya ya ilala, na kushoto ni Musatafa Hassanali, mjasiriamali mbunifu na muasisi wa TWENDE


Washiriki wa TWENDE 2011, wakisalimiana na Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami mara baada ya waziri huyo kuwatembelea katika banda lao na kujionea bidhaa wanazotengeneza

Washiriki wa Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Tanzania- TWENDE, 2011, kutoka mikoa tofauti ya Tanzania na nje ya nchi wakionyesha bidhaa zao katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam

 TWENDE 2012 KUFANYIKA KWA MWAKA WA TATU SASA · SEMINA NA MAONESHO YA TWENDE NI KUANZIA TAREHE 18 HADI 20 YA MWEZI WA KUMI KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM. · WANAWAKE WAJASIRIAMALI KUELIMIKA, KUUZA BIDHAA ZAO NA KUKUZA MTANDAO WA KIBIASHARA KUPITIA JUKWAA LA WANAWAKE WAJASIRIAMALI TANZANIA- TWENDE
 Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Tanzania- TWENDE linatarajia kufanyika kuanzia tarehe 18 – 20 ya mwezi wa kumi 2012 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. TWENDE imekuwa ikifanyika kila mwaka kwa mwaka watatu sasa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2010, lengo likiwa ni kuwaleta pamoja wanawake wajasiriamali wadogo, wakubwa na wale wanaochipukia ili kupata fursa ya kuuza, kuonesha na kujadili masuala ya biashara kwa ujumla. Sambamba na hilo. TWENDE inalenga kusaidiana na serikali katika kutimiza malengo ya milenia likiwemo lengo namba moja ambalo linalenga kuondoa umasikini, namba tatu kutetea haki na fursa sawa kwa wanawake, lengo namba tano kuhamasisha afya ya uzazi na lengo namba nane, ambayo ni kuendeleza uhusiano wa kudumu kwa ajili ya maendeleo ya jamii. Pia TWENDE inalenga Kukuza uzalishaji kwa wanawake wafanyabiashara na kukuza mgawanyiko wa masoko sambamba na muonekano wa wafanyabiashara wanawake katika jamii. Kwa upande wa mwaka huu TWENDE inatarajia kuwashirikisha wanawake wajasiriamali wengi zaidi ambao wamekuwa wakifanya biashasha tofauti ili kuweza kupata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuongeza ujuzi zaidi kibiashara. Sambamba na semina bora zitakazotolewa kwa wanawake wote ambao watapata elimu itakayotolewa wataalamu wa fani mbalimbali Kwa miaka mitatu mfululizo TWENDE imekuwa ikitoa fursa kwa wanawake wajasiriamali kukutana pamoja na kujadili mafanikio na changamoto ambazo zimekuwa ni kikwazo cha wanawake wajasiriamali kutofikia malengo yao kibiashara. “Licha ya kwamba wanawake wengi wamejikita katika sekta hii ya ujasiriamali, lakini bado wamekuwa wakikabiliawa na changamoto mbalimbali zinazokwamisha kufikia malengo yao, ikiwemo elimu ya ujasiriamli na upatikanaji wa mikopo, kwa hiyo ipo haja kwa wanawake kujijengea utaratibu wa kushiriki katika fursa kama hizi zinazowajengea uwezo”. Alisema Saphia Ngalapi Meneja Mradi wa TWENDE. Zaidi ya Wanawake Wajasiriamali Wanawake 100 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani wanatarajai kushiriki katika TWENDE mwaka huu, ampabo maonesho hayo yanakwenda sambamba na semina zitakazo tolewa kwa wanawake wote bure, kwa wale watakaoshiriki katika maonesho, na hata wale ambo watakuwa hawakupata frusa ya kuonesha na kuuza bidhaa zao. KUHUSU TWENDE Tanzania Women Entrepreneurs & Networking Development Exposition (TWENDE) inapanga kuleta maendeleo kwa wanawake wajasiriamali kwa kuandaa jukwaa ambalo litakua mahususi kuweza kukutana zaidi ya wanawake wafanyabiashara 100 wadogo, wakati na wakubwa kutoka viwanda vikubwa na vidogo, taasisi za serikali na mashirika yasio ya kiserikali (NGO). Tanzania Women Entrepreneurs & Networking Development Exposition (TWENDE) pia inalenga kuyapa fursa makampuni kukutana yakikidhi malengo ya wahudhuriaji. Ni sehemu ya kuuza na kuonyesha bidhaa na huduma za kampuni mbalimbali kwa wafanya maamuzi. Maonyesho haya yataenda sambamba na mkutano wa siku tatu utakaotoa elimu bora kwa washiriki. MTAZAMO WA TWENDE Ni kuwaelimisha kuwahamasisha na kuwaendeleza wanawake Tanzania.

MWAMVITA MAKAMBA AHIMIZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KUTUMIA VEMA FURSA


Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akiongea na wakina mama wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani  Manyara, mara alipofika kijijini hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama,ambapo urudishwa kwa njia ya m-pesa bila riba,Mikopo hiyo huendeshwa na Mfuko wa kampuni hiyo MWEI kupitia Vodacom Foundation,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000)


Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akimkabidhi mmoja wa kinamama wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani  Manyara,fedha za  mkopo  unaolenga kuwakomboa wakinamama hapa nchini, Huduma hiyo hutolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa (MWEI) na kurudisha fedha hizo bila riba kwa njia ya m-pesa,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000)


Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akimshuhudia Glory Muro, wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani  Manyara,akisaini nyaraka za kupewa mkopo wa kifedha  inayolenga kuwakomboa wakinamama hapa nchini, Huduma hiyo hutolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa kusaidia kinama wa (MWEI) na kurudisha fedha hizo bila riba kwa njia ya m-pesa,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000)kulia ni Afisa wa Mradi huyo….


Bi.Johari Mwaselela wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani  Manyara,akisaini nyaraka za kupewa mkopo wakati  Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wapili toka kulia alipofika  kijijini hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama,Huduma hiyo ya Mikopo hutolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa kusaidia wakinama MWEI na kurudishwa kwa njia ya m-pesa bila riba,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000)kulia ni Afisa wa Mradi huyo Ally Mbuyu,na kushoto ni Meneja wa Mradi huo Mwamvua Mlangwa.


Baadhi ya kinamama wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani  Manyara, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Ofisa Mkuu na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wanne toka kushoto na Meneja wa Mradi wa MWEI Mwamvua Mlangwa mara baada ya kufika hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama kijijini hapo,Mikopo hiyo urudishwa bila riba kwa njia ya m-pesa,Huduma hiyo hutolewa na Vodacom Foundation kwa kupitia Mradi wao wa  MWEI,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000)

Baadhi ya kinamama wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani  Manyara, wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakiongea na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,(hayupo pichani) mara alipofika kijijini hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama,Mikopo hiyo urudishwa kwa njia ya m-pesa bila riba,Huduma hiyo hutolewa na Vodacom Foundation kupitia Mradi wa MWEI,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000)
---
·         Akabidhi mikopo nafuu kwa vikundi tisa vya Mirerani
·         Ni kupitia mradi wa MWEI

Na Mwandishi wetu.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Bi. Mwamvita Makamba amewataka wanawake wajasiriamali hususan wadogo kutambua kuwa maendeleo ya biashara zao na hatimae hali zao za kiuchumi kutategemea pamoja na mambo mengine namna wanavyotumia vizuri fursa za uwezeshaji wanazotengenezewa.

Bi. Mwamvita ametoa changamoto hiyo Wilayani Simanajiro, Mkoani Manyara katika kijiji Cha Mirerani wakati akikabidhi mikopo isiyo na riba wala dhamana yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni Tisa kwa vikundi tisa vya akina mama iliyotolewas na mradi wa Vodacom wa kusaidia wajasiriamali wadogo wanawake wa MWEI.

Bi. Mwamvita amesema kadiri ambavyo wanawake watakuwa tayari kutumia vema fursa wanazotengenezewa ikiwemo ya MWEI wanajiweka katika nafasi nzuri ya kujiwezesha kiuchumi na kuondokana na dhana kwamba mwanamke ni kiumbe tegemezi.
“Wanawake wenzangu leo Vodacom inapowakabidhi mikopo isiyo na riba wala dhamana ni fursa adhimu sana kwenu, ni wajibu wenu kutumia vema fursa hii kujiinua kama ilivyokuwa wajibu wa Vodacom kuwatafuta, kuwafikia na kuwawezesha, kazi sasa ni kwenu”Alisema Bi. Mwamvita.

Bi. Mwamvita amesema kumekuwepo na kilio kikubwa cha wanawake wajasiriamali wadogo kutofikiwa kwa urahisi ama kukosa uwezo wa kukopesheka kutoka taasisi za fedha, hivyo katika kutimiza azma ya kubadili maisha ya watanzania Vodacom ilibuni mradi wa MWEI kutatua changamoto hiyo.

“Ni vigumu kupata taasisi itakayokukopesha mfnyabishara wa vitumbua, genge mchuuzi wa samaki, msusi n.k tena bila riba wala dhamana na zaidi kukupatia mafunzo ya ujasiriamali kwa gharama zake, Vodacom licha ya kwamba biashara yetu ni huduma za simu imethubutu kubuni mradi wa mikopo kwa kuwa inapenda kuona maisha ya watanzania wakiwemo akina mama yanabadilika”Aliongeza Mwamvita

Aidha Bi. Mwamvita amewataka wanawake hao kuhakikisha mikopo waliyoichukua inleta tija katika biashara zao hasa kuinua mitaji ili nao waweze kusimama na kusaidia wanawake wengine.

“Kabla ya kuwakibidhi mikopo hii tumewapatia mafunzo ya ujasiriamali ikiwemo somo la utunzaji wa mahesabu ya biashara, tutumie elimu hiyo na mikopo hii kujiimarisha ili kuinua sauti zetu kwenye jamii”Aliongeza Mwamvita huku akisindikizwa na vigelegele vya furaha kutoka kwa akina mama. 

Mradi wa MWEI ni mahsusi kwa ajili ya kusaidia akina mama nchini kama mchango wa Vodacom kuunga mkono juhudi za kitaifa za kumwezesha kiuchumi mwanamke wa kitanzania na unalenga hasa wanawake wenye biashara zenye mitaji ya  kati ya Sh. 5000 na 200,000
Bi. Mwamvita amesema kuwa mradi wa MWEI umejiwekea lengo la kuwafikia wanawake wengi zaidi hususan maeneo ya vijijini ambao pamoja na kujituma katika bishara ndogondogo wanakabiliw ana uchache wa fursa za uwezeshaji.

“Ni hatua muhimu katika maisha yetu kama Vodacom kusaidia ujenzi wa ustawi wa jamii hapa nchini, tuna namna nyingi ya kubadili maisha ya watanzania kama  dira yetu invyosema, MWEI ni namna mojawapo”. Alisema Mwamvita.

Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa mikopo hiyo mbali na kuishukuru Vodacom, wanufaika hao wameahidi kuitumia vizuri mikopo hiyo ili kutimiza malengo ya kibiashara waliyonayo.

“Wengi wetu hapa ni wajasiriamali wadogo tunaojishughulisha na biashara za ususi, mama lishe n.k changamoto kubwa tuliyokuwa tukikabiliana nayo ni kuweza kufikiwa na mikopo nafuu, leo tunafuraha kuona tumepata mikopo isiyo na riba hata shilingi moja” Alisema Johari Mwaselela Mmoja wa viongozi wa Vikundi.

Amesema kupitia vikundi vyao, watahakikisha wanafanya kazi kwa pamoja na kuhimizana ili mikopo waliyopatiwa itoe tija ya kuinua mitaji yao, wakuze faida sambamba na kusaidia kubadili hali zao za maisha.

Tunawaomba Vodacom kama mlivyotufikia sisi hapa kijijini muwafikie na wenzetu wengine waliopo vijijini kama sisi na muwaokoe, kwa kweli wanawke bado tupo nyuma, tunawashukuru sana MWEI.”Aliongeza Mamam Mwaselela.

Awali Meneja wa Mradi wa MWEI Bi Mwamvua Mlangwa alisema hadi kufikia Januari mwaka huu kiasi cha Shilingi 150 Milioni kimeshatolewa na kunufaisha akina mama zaidi ya 6,000
Bi. Mwamvua amesema idadi ya wanaohitaji mikopo hiyo ni kubwa hivyo amewasihi kina mama hao wa Mirerani kutumia vizuri fursa hiyo na kuhakikisha wanarudisha mikopo kwa wakati ili kuwafikia wanawake wa sehemu nyengine nchini.
Kupitia mradi wa MWEI Vodacom huvipatia vikundi vya akina mama mikopo  pamoja na mafunzo ya ujasiriamali kazi ambayo hufanywa na Shirika la kuhudumia viwanda Vidogo – SIDO kwa gharama za Vodacom.

Mikoa ya Arusha, Manyara, Morogoro, Tanga, Rukwa na Katavi, Dodoma, Mara, Mwanza,Shinyanga na Pwani imeshanufaika na mikopo ya MWEI tangu mradi huo ulipoanzishwa mwaka 2011.