Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akiongea na wakina mama wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mara alipofika kijijini hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama,ambapo urudishwa kwa njia ya m-pesa bila riba,Mikopo hiyo huendeshwa na Mfuko wa kampuni hiyo MWEI kupitia Vodacom Foundation,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000)
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akimkabidhi mmoja wa kinamama wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,fedha za mkopo unaolenga kuwakomboa wakinamama hapa nchini, Huduma hiyo hutolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa (MWEI) na kurudisha fedha hizo bila riba kwa njia ya m-pesa,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000)
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akimshuhudia Glory Muro, wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,akisaini nyaraka za kupewa mkopo wa kifedha inayolenga kuwakomboa wakinamama hapa nchini, Huduma hiyo hutolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa kusaidia kinama wa (MWEI) na kurudisha fedha hizo bila riba kwa njia ya m-pesa,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000)kulia ni Afisa wa Mradi huyo….
Bi.Johari Mwaselela wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,akisaini nyaraka za kupewa mkopo wakati Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wapili toka kulia alipofika kijijini hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama,Huduma hiyo ya Mikopo hutolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa kusaidia wakinama MWEI na kurudishwa kwa njia ya m-pesa bila riba,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000)kulia ni Afisa wa Mradi huyo Ally Mbuyu,na kushoto ni Meneja wa Mradi huo Mwamvua Mlangwa.
Baadhi ya kinamama wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Ofisa Mkuu na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wanne toka kushoto na Meneja wa Mradi wa MWEI Mwamvua Mlangwa mara baada ya kufika hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama kijijini hapo,Mikopo hiyo urudishwa bila riba kwa njia ya m-pesa,Huduma hiyo hutolewa na Vodacom Foundation kwa kupitia Mradi wao wa MWEI,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000)
Baadhi ya kinamama
wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakifurahia
jambo wakati walipokuwa wakiongea na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano
wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,(hayupo pichani) mara alipofika
kijijini hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya
kinamama,Mikopo hiyo urudishwa kwa njia ya m-pesa bila riba,Huduma hiyo
hutolewa na Vodacom Foundation kupitia Mradi wa MWEI,zaidi ya kinamama
108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki
saba,(9,700,000)
---
·
Akabidhi
mikopo nafuu kwa vikundi tisa vya Mirerani
· Ni kupitia mradi wa MWEI
Na Mwandishi
wetu.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom
Bi. Mwamvita Makamba amewataka wanawake wajasiriamali hususan wadogo
kutambua kuwa maendeleo ya biashara zao na hatimae hali zao za kiuchumi
kutategemea pamoja na mambo mengine namna wanavyotumia vizuri fursa za
uwezeshaji wanazotengenezewa.
Bi. Mwamvita ametoa changamoto hiyo Wilayani
Simanajiro, Mkoani Manyara katika kijiji Cha Mirerani wakati akikabidhi
mikopo isiyo na riba wala dhamana yenye thamani ya zaidi ya Shilingi
Milioni Tisa kwa vikundi tisa vya akina mama iliyotolewas na mradi wa
Vodacom wa kusaidia wajasiriamali wadogo wanawake wa MWEI.
Bi. Mwamvita amesema kadiri ambavyo wanawake
watakuwa tayari kutumia vema fursa wanazotengenezewa ikiwemo ya MWEI
wanajiweka katika nafasi nzuri ya kujiwezesha kiuchumi na kuondokana na
dhana kwamba mwanamke ni kiumbe tegemezi.
“Wanawake
wenzangu leo Vodacom inapowakabidhi mikopo isiyo na riba wala dhamana ni
fursa adhimu sana kwenu, ni wajibu wenu kutumia vema fursa hii kujiinua
kama ilivyokuwa wajibu wa Vodacom kuwatafuta, kuwafikia na kuwawezesha,
kazi sasa ni kwenu”Alisema Bi. Mwamvita.
Bi. Mwamvita amesema kumekuwepo na kilio
kikubwa cha wanawake wajasiriamali wadogo kutofikiwa kwa urahisi ama
kukosa uwezo wa kukopesheka kutoka taasisi za fedha, hivyo katika
kutimiza azma ya kubadili maisha ya watanzania Vodacom ilibuni mradi wa
MWEI kutatua changamoto hiyo.
“Ni vigumu kupata taasisi itakayokukopesha
mfnyabishara wa vitumbua, genge mchuuzi wa samaki, msusi n.k tena bila
riba wala dhamana na zaidi kukupatia mafunzo ya ujasiriamali kwa gharama
zake, Vodacom licha ya kwamba biashara yetu ni huduma za simu
imethubutu kubuni mradi wa mikopo kwa kuwa inapenda kuona maisha ya
watanzania wakiwemo akina mama yanabadilika”Aliongeza Mwamvita
Aidha Bi. Mwamvita amewataka wanawake hao
kuhakikisha mikopo waliyoichukua inleta tija katika biashara zao hasa
kuinua mitaji ili nao waweze kusimama na kusaidia wanawake wengine.
“Kabla ya kuwakibidhi mikopo hii tumewapatia
mafunzo ya ujasiriamali ikiwemo somo la utunzaji wa mahesabu ya
biashara, tutumie elimu hiyo na mikopo hii kujiimarisha ili kuinua sauti
zetu kwenye jamii”Aliongeza Mwamvita huku akisindikizwa na vigelegele
vya furaha kutoka kwa akina mama.
Mradi wa MWEI ni mahsusi kwa ajili ya
kusaidia akina mama nchini kama mchango wa Vodacom kuunga mkono juhudi
za kitaifa za kumwezesha kiuchumi mwanamke wa kitanzania na unalenga
hasa wanawake wenye biashara zenye mitaji ya kati ya Sh. 5000 na
200,000
Bi. Mwamvita amesema kuwa mradi wa MWEI
umejiwekea lengo la kuwafikia wanawake wengi zaidi hususan maeneo ya
vijijini ambao pamoja na kujituma katika bishara ndogondogo wanakabiliw
ana uchache wa fursa za uwezeshaji.
“Ni hatua muhimu katika maisha yetu kama
Vodacom kusaidia ujenzi wa ustawi wa jamii hapa nchini, tuna namna
nyingi ya kubadili maisha ya watanzania kama dira yetu invyosema, MWEI
ni namna mojawapo”. Alisema Mwamvita.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa mikopo
hiyo mbali na kuishukuru Vodacom, wanufaika hao wameahidi kuitumia
vizuri mikopo hiyo ili kutimiza malengo ya kibiashara waliyonayo.
“Wengi wetu hapa ni wajasiriamali wadogo
tunaojishughulisha na biashara za ususi, mama lishe n.k changamoto kubwa
tuliyokuwa tukikabiliana nayo ni kuweza kufikiwa na mikopo nafuu, leo
tunafuraha kuona tumepata mikopo isiyo na riba hata shilingi moja”
Alisema Johari Mwaselela Mmoja wa viongozi wa Vikundi.
Amesema kupitia vikundi vyao, watahakikisha
wanafanya kazi kwa pamoja na kuhimizana ili mikopo waliyopatiwa itoe
tija ya kuinua mitaji yao, wakuze faida sambamba na kusaidia kubadili
hali zao za maisha.
Tunawaomba Vodacom kama mlivyotufikia sisi
hapa kijijini muwafikie na wenzetu wengine waliopo vijijini kama sisi na
muwaokoe, kwa kweli wanawke bado tupo nyuma, tunawashukuru sana
MWEI.”Aliongeza Mamam Mwaselela.
Awali Meneja wa Mradi wa MWEI Bi Mwamvua
Mlangwa alisema hadi kufikia Januari mwaka huu kiasi cha Shilingi 150
Milioni kimeshatolewa na kunufaisha akina mama zaidi ya 6,000
Bi. Mwamvua
amesema idadi ya wanaohitaji mikopo hiyo ni kubwa hivyo amewasihi kina
mama hao wa Mirerani kutumia vizuri fursa hiyo na kuhakikisha
wanarudisha mikopo kwa wakati ili kuwafikia wanawake wa sehemu nyengine
nchini.
Kupitia mradi wa MWEI Vodacom huvipatia
vikundi vya akina mama mikopo pamoja na mafunzo ya ujasiriamali kazi
ambayo hufanywa na Shirika la kuhudumia viwanda Vidogo – SIDO kwa
gharama za Vodacom.
Mikoa ya Arusha, Manyara, Morogoro, Tanga,
Rukwa na Katavi, Dodoma, Mara, Mwanza,Shinyanga na Pwani imeshanufaika
na mikopo ya MWEI tangu mradi huo ulipoanzishwa mwaka 2011.
Huu ni mpango mzuri sana katika uwezeshaji akina mama.
ReplyDelete