Idadi ya wanyama wanaofugwa kwa
chakula imezidi ile ya binadamu zaidi ya mara mbili kote ulimwenguni. Kuna maelfu ya wanyama kote duniani
ilihali ni wachache tu wanaoweza kufugwa. Kati ya hawa wanyama, ni aina nne
(Ng'ombe, kondoo, mbuzi na kuku) wanaochukua asilimia 95% ya wanyama wote
wanaofugwa. Wanyama hawa hupatikana katika nchi za hari kwenye nyanda za chini.
Lakini kati ya mifugo hawa, kuku ni maarufu katika nchi za hari na hata kote
ulimwenguni.
Lengo la
makala haya ni kutoa maelezo ili kusaidia wafugaji wa kiwango kidogo katika
nchi
zinazostawi,
katika kupunguza umaskini. Sehemu ya kwanza (I) itatoa maelezo kuhusu ufugaji
na hasa ufugaji
wa kuku, Sehemu ya pili (II) itaangazia maswala yafuatayo katika kuinua hali ya
uchumi kwa kufuga
kuku:
1.
Kuendeleza ufugaji wa kuku za kienyeji kwa kutumia njia zisizohitaji gharama
nyingi.
2. Kutafuta
mbinu na njia muafaka za kuzalisha viwango vya kuku bora kwa njia ya
kiasili.
3. Matumizi
ya njia za kiasili au zile zisizo gharimu pesa nyingi kutibu na kuzuia magonjwa
ya kuku.
SEHEMU YA
I: MAELEZO KUHUSU UFUGAJI WA KUKU KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA
NAFASI YA
MIFUGO
Licha ya
kukosa mashamba makubwa ya kuendeleza ufugaji wa ng'ombe, jamii nyingi katika
nchi za hari
(tropics) hupata nafasi ya kufuga kuku kwa kiwango kidogo.
Idadi ya wanyama
wanaofugwa huongezeka
sambamba na ile ya watu. Idadi ya watu inapoongezeka ndipo ile ya mifugo
huzidi.
Idadi kubwa
ya watu huhitaji chakula kingi na matumizi huongezeka, hivyo basi watu hufanya
bidii kuzalisha
chakula na mapato kutoka kwa shamba.
Ufugaji wa
ng'ombe na wanyama wanaohitaji lishe kwa wingi huhitaji kiasi kikubwa cha shamba
ili kupanda
mimea na lishe la mifugo. Ukilinganisha na ufugaji wa kuku, utahitaji mabaki ya
vyakula na sehemu
ndogo ya shamba. Ufugaji wa kuku umeweza kunawiri hata pasipo
fedha.
Katika nchi
za hari ufugaji wa kienyeji hautahitaji kazi nyingi, kazi hii hufanywa na akina
mama na watoto. Kwa
kawaida katika nchi hizi kazi nyingi za nyumbani hutekelezwa na mama. Vyakula
vya kuku vyaweza
kutoka kwa: 1) Mabaki ya chakula, 2) Mabaki ya mimea, 3) Mabaki kutoka
jikoni na 4)
Vyakula vya kujitafutia (kwa mfano kwekwe, mbegu, wadudu, nyongonyongo, n.k).
Mfumo wa kufuga
kuku kwa njia ya kienyeji hutumia viungo vinavyopatikana kwa urahisi na
kuimarisha hali ya kiuchumi
na chakula bora kwa jamii.
Ni muhimu
sana kufuga mifugo hata ikiwa ni kwa kiwango kidogo kwa sababu ya 1) Chakula
bora na kuongeza
mapato ya jamii kwa viwango vya kuridhisha; 2) Mifugo ni hakiba au banki, faida
yakehuzaana tu
kama riba ya benki; 3) Mifugo yaweza kuuzwa ili kugharamia karo ya
wanafunzi,malipo ya
hospitali, gharama nyingine za nyumbani na hata shambani; 4) Kwa matumizi ya
kijamii (kwa mfano
kulipia mahari, shughuli za kidini, n.k); 5) Mifugo husaidia katika kukabili
wadudu,kwekwe na
kuimarisha rutuba kutokana na mbolea ya kinyesi. Ni bayana kwamba mifugo
ni muhimu
sana kwa mkulima yeyote yule.
UMUHIMU WA
UFUGAJI WA NJIA YA KIENYEJI
Ufugaji wa
kuku katika nchi zinazostawi waweza kugawanywa mara mbili: 1) Ufugaji
wa
kitamaduni
au kienyeji pasipo kuwepo gharama, na 2) Ufugaji wa kisasa unaohitaji fedha
nyingi.
Ufugaji wa
viwango vikubwa kwa kuzingatia mfumo wa kisasa ni maarufu katika kuzalisha kuku
wa nyama na
wale wa mayai. Mfumo huu hujumuisha asilimia ndogo sana ya aina ya
ufugaji.
Itafahamika
kwamba mfumo wa kisasa haujaadhiri ule wa kienyeji. Idadi kubwa ya watu katika
nchi za hari
hutegemea mfumo wa kienyeji kwa nyama na mayai.
Mfumo wa
kisasa huhitaji pesa nyingi za kununua vyakula vya kuku. Aidha mfumo wa kisasa
huhitaji kazi nyingi ili kutekeleza. Mfumo wa kisasa umefaulu
katika nchi zilizostawi kutokana na hali nzuri ya kiuchumi katika kuzalisha
(kuku wa hali ya juu,
kuangua vifaranga kwa stima, vyakula vilivyo na madini mengi, vifaa na zana za
mashine,utaalamu wa
hali ya juu n.k). Haitafaa sana kuanzisha mfumo kama huu katika vijiji vya
mataifa yanayostawi.
"Mageuzi"
katika ufugaji (kuambatanisha mfumo wa kisasa pamoja na ule wa kienyeji)
yamefanyiwa majaribio
katika mataifa yanayostawi tangu miaka ya 1950.
Matokeo ya kuku wapatao 200 hadi
300kwa shamba
moja hayajawai kufaulu. Hasara imepatikana na waweza kuona nyumba zilizokuwa
na kuku bila
chochote, pesa nyingi zimepotea na kuku hawapo.
Mfumo wa
kienyeji ni bora (Katika hali ya kiuchumi) iwapo idadi ya kuku haitazidi kuku
50. Ni rahisi
kuweza kuwatunza kuku, kwani hakuna gharama nyingi. Iwapo vyakula au zana za
kisasa zitanunuliwa, basi haitakuwa kwa viwango vikubwa. Mazao ya nyama
na mayai yataleta faida.
Sehemu
nyingi katika mataifa yanayostawi hakuna stima, katika nchi za hari, ufugaji kwa
kiwangokidogo
umeweza kufaulu na kuimarisha uchumi.
FAIDA ZA
UFUGAJI WA KUKU KWA NJIA YA KIENYEJI
Faida za
uzalishaji kuku ili kuimarisha uchumi kwa njia hii zimepuuzwa na viongozi na
wafadhili.
Kuku huleta
faida kwa jamii kama tulivyoona katika sehemu ya I. Zaidi ya hayo, ufugaji wa
kuku waweza kuimarishwa pasipo gharama nyingi ukilinganisha na mifugo
wengine.
· Hutupatia fedha kwa kuuza
nyama na mayai
· Mayai ni chakula kilicho na
madini muhimu na kisicho ghali katika soko lolote. (madini kama methionine
na cystine), madini haya ni muhimu sana kwa afya ya watu hasa watoto
wachanga. Pia hutupatia protini.
· Kinyesi cha kuku ni mbolea
safi
· Kiwanda asilia cha kutotoa
vifaranga
· Gharama za kuanzisha na
kuendeleza ni nyepesi
· Kitoweo chepesi na rahisi kwa
wageni, kitoweo hakihitaji hifadhi hutumika mlo mmoja au miwili na
kumalizika
· Jogoo hutumika kama saa
inapowika
· Manyoya ya kuku hutumika
kutengenezwa mapambo mbalimbali, mito na magodoro
·
Kuku wanahisimu wadudu waharibifu
Kuku ndiye
mnyama wa kipekee anayeweza kuishi mahali popote hapa ulimwenguni bila
kuadhiriwa
na viwango
vya hali ya hewa. Ufugaji wa kuku ndio shughuli inayofanyika kwa wingi duniani
kuliko ufugaji wa aina yeyote. Kuku hunawiri vyema katika nchi za hari kutokana
na uwiano uliopatikana wakati wa mwanzo binadamu alipofuga Asian jungle fowl
aina ya kuku-mwitu. Mayai pia yaweza kuhifadhiwa kwa urahisi na huchukua
nafasi ndogo kuliko aina ya bidhaa zozote za mifugo. Mayai yaweza kuwekwa mahali
kwa muda mrefu bila kuhitaji barafu. Hautahitaji kuhifadhi kuku kwa njia yoyote,
kwani nyama yake hupatikana pale unapohitaji kwa kuchinja.
Upungufu wa
kuku wa kigeni ukilinganisha na wale wa kienyeji ni kama ufuatao:
• Kuku wa
kigeni hawawezi kukalia na kuangua mayai, hivyo basi wahitajika kununua
vifaranga (gharama);
• Vifaranga
wa kigeni huhitaji utunzaji maalum na vyakula maalum (gharama);
• Kuku
waliozalishwa kwa njia ya kisasa huhitaji chakula kingi ili kutaga mayai
(gharama);
• Kuku wa
kisasa huhitaji zaidi kuchanjwa dhidi ya magonjwa (gharama)ukilinganisha na wa
kienyeji (japo nao huhitaji chanjo);
• Kuku wa
kutaga mayai huhitaji mwangaza wa stima (saa 14 kwa siku) ili kutaga mayai
(gharama)
Kwa
kuongezea, rangi ya nyama na mayai ya kuku wa kienyeji huvutia kuliko ile ya
kuku wa kisasa.
Hivyo basi
jaribu kuendeleza na kuhimiza ufugaji wa kuku wa kienyeji.
Iwapo
mkulima ana jogoo mmoja na kuku kumi na mbili, basi kila mwezi waweza kupata
kuku akikalia
mayai 10-12 kwa mwezi (mayai yote kwa wakati mwingi hayataanguliwa) kuna
hakikisho la kupata
vifaranga vinne kila mwezi. Kuku mzima atachukua miezi minne kuchunga
vifaranga walioanguliwa.
Kwa hivyo, kati ya kuku wote kumi na mbili kila
mara kutakuwa na kuku wanne wakitunza
vifaranga, huku wale wengine wanane wakitaga mayai.
Kuku
waliofugwa kwa njia ya kitamaduni hupata vyakula vyao kwa kutafuta mbegu,
wadudu
nyongonyongo, n.k; Lakini kuku hawa hukosa vyakula vya kutosha
vilivyo na nguvu ili waweze kutaga mayai. Vyakula vya kutoa nguvu daima huwa ni
haba.
Waweza
kuwalisha kuku kwa nafaka ili wapate chakula cha nguvu (mfano kilo moja ya
nafaka iliyopondwa
kila siku kwa kuku 10), nafaka hii yapaswa kuwa kavu. Vifaranga wapewe kiasi
kidogo cha nafaka
au mchele wiki za kwanza. Kuku wanaolishwa nafaka baada ya kujitafutia chakula
nje huongeza
idadi ya mayai (kutoka asilimia 20-25% hadi 40-50%). Kuna umuhimu wa
kuhifadhi nafaka kama
lishe badala ya kuuza kwani utapata mayai mengi ambayo baadaye utaweza
kuuza.
Hautahitaji
kununua vyakula vya protini kwani kuku hujitafutia lishe la
protini.
Ikiwa hauna
nafaka, waweza kutumia vyakula vya mzizi au ndizi. Vyakula vya aina hii hata
hivyo, huwatatiza
kuku wanapovitonogoa, kiwango cha mayai sio kikubwa kama cha wale
wanaolishwa nafaka.
Kwa
kuwalisha kuku kwa nafaka utapata hakikisho la mayai manne kwa siku kutoka kwa
wale kuku wanane.
Iwapo hakuna nafaka, kati ya kuku wanane wanaotaga utapata mayai mawili tu kwa
siku.
Ni bora
kutumia nafaka hii kama lishe kuliko kuuza na hatimaye kununua vyakula vya
dukani.
Kuku kumi na
mbili na jogoo mmoja wanaolishwa kwa kilo moja ya nafaka kila siku
waweza
kuelezwa
hivi:
• Waweza
kuuza kuku wanne kila mwezi na kujaza pengo hilo na wale vifaranga
(vifaranga
wanne
huanguliwa kila mwezi) na
• Dazani
kumi za mayai kila mwezi (mayai manne kila siku).
Kwa mwaka
mmoja waweza kukadiri ile faida utakayopata na vile hali ya kiuchumi
yaweza
kuinuliwa katika mataifa
yanayostawi.
Hata hivyo
faida hii haitaafikiwa iwapo magonjwa
hayatazuiwa
au kukabiliwa kama ifuatavyo.
TEKELEZA
UTARATIBU WA KUZUIA MAGONJWA
Magonjwa
ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi
ya magonjwa
hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora
kuliko kuponya.
Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu) dhidi ya
magonjwa yafuatayo:
Ugonjwa
wa Newcastle
Ugonjwa huu
ndio huadhiri kuku na kusababisha hasara katika nchi za hari. Virusi vya ugonjwa
huu huenea kwa
kasi na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%. Dalili za kwanza ni
shida ya kupumua
na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate. Kinyesi chaweza
kuwa na rangi ya
kijani kibichi. Hadi sasa hakuna dawa.
Waweza
kuzuia ugonjwa huu kwa kutoa chanjo. Dawa za chanjo hupatikana kote ulimwenguni
hata katika nchi
za hari kwenye vipimo vya vitone mia moja. Madawa haya yaweza kuhifadhiwa
kwa muda. Waweza
kuweka kwa wiki moja mbali na jua au joto kali (Chanjo hii ni ya kipekee,
kwani aina
nyingine ya chanjo huwekwa kwa friji). Waweza kutoa chanjo kwa kutia vitone
kwenye mdomo. Kuku wote (wakubwa kwa wadogo) wapaswa kupewa
chanjo baada ya kila miezi mitatu.
Minyoo
Minyoo kama
chango (roundworms) na tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji.
Kuku hukosa hamu ya chakula, mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia. Ni
bora basi kutoa minyoo.
Mchanganyiko
wa madawa ya aina tatu ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya
ni piperazine, phenothiazine na butynorate. Madawa
haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1 kwa kuku
mzima na 1/2 kwa vifaranga). Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur
au dawa
nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi
mitatu.
Wadudu
Wadudu kama
chawa au utitiri husumbua kuku katika ufugaji wa kienyeji. Chawa au
utitiri
husababisha
harara ya ngozi, kuku walio adhiriwa hupata shida na kukosa usingizi. Hali
hii
hupunguza
kiwango cha mayai na uzito wa kuku.
Tumia
asilimia 5% ya unga wa malathion kwa kupulizia kuku (puliza kwa chupa
uliyo toboa
mashimo)
pulizia kila kuku ili kuzuia chawa na utitiri (kilo moja ya unga huu yaweza
kutibu kuku 150).
Pulizia dawa hii baada ya kila miezi mitatu, waweza kupuliza kwa wakati mmoja wa
kutoa chanjo na
dawa zilizotajwa hapo juu. Puliza unga huu pia kwenye viota vya kuangulia
mayai.
Waweza
kutayarisha 5% ya malathion kwa kuchanganya 25% ya unga wa malathion
(kiwango cha kilimo) na
sehemu nne za jivu kutoka jikoni.
Magonjwa
ya mapafu
Magonjwa ya
mapafu huadhiri njia inayopitisha hewa na kuambatanisha mate na sauti kama
ya kikohozi.
Ugonjwa huu huenea polepole. Uambukizanaji pia hutokea kwa polepole na vifo sio
kwa wingi.
Hata
hivyo, kutaga mayai na uzito hupungua. Shida hii yaweza kusambaa hata kutoka
mahali vifaranga huanguliwa hadi pale walipouzwa.
Tylosin19 ndio dawa inayoweza kutibu magonjwa ya mapafu.
Kiasi cha 35mg ya tylosin hutosha kuku mmoja
(kiwango hiki hufaa kuku na hata vifaranga) dawa hii husimamisha madhara
kutokana na magonjwa
ya mapafu.
Tibu kuku kila baada ya miezi mitatu, waweza kutekeleza kwa
wakatimmoja wa
kutoa kinga na kuangamiza minyoo. Tylosin hupatikana kwa pakiti ndogo ya
4gm.
Waweza
kutayarisha dawa hii kwa kutumia maji na 35gm ya tylosin (gramu nne kwa
vikombe viwili vya maji),
kiasi hiki chaweza kutolewa kwa vitone kwa kila kuku.
KWA
UFUPI (SUMMARY)
Kabila
za Kuku
Si
rahisi kupata kabila halisi (pure breed) au kizazi halisi (pure line) za kuku wa
kienyeji kutokana na mwingiliano wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao.
Lakini hata hivyo baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kutokana na
maumbile yao kwa mfano
1.
Kuchi
-
Warefuna wenye kusimama mgongo ukiwa wima
-
Wana
manyoya machache mwilini na vilemba vyao ni vidogo
-
Majogoo huwa na wastani wa kilo 2.5 na mitetea kilo
1.8
-
Mayai gram 45
2.
Ching'wekwe (Umbo dogo)
3.
Umbo la Kati
4.
Singamagazi
5.
Mbeya
6.
Pemba
7.
Unguja
SIFA
WA KUKU WA KIENYEJI
-
Wastahimilivu wa Magonjwa
-
Wana
uwezo wa kujitafutia chakula
-
Huatamia, kutotoa na kulea vifaranga
-
Wanastahimili mazingira magumu(ukame, baridi
n.k)
-
Nyama yake ina ladha nzuri
KATIKA
KUWAENDELEZA KUKU WA KIENYEJI NI VYEMA
-
Wajengewe nyumba bora
-
Wapewe kinga dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle), Ndui
(Fowl Pox) pamoja na kinga ya minyoo.
-
Malezi bora ya vifaranga
-
Kuwapatia chakula cha ziada pamoja na maji ya kunywa ya
kutosha.
NYUMBA
BORA
Eneo
inapojengwa nyumba au banda la kuku liwe
Vifaa
kama miti, nyasi, makuti, fito, udongo mabanzi ya miti, cement, mabati
n.k
Sifa
za Nyumba Bora ya Kuku
-
Paa
imara lisilovuja
-
Kuta
zisiwe na nyufa
-
Sakafu isiwe na nyufa
-
Madirisha ya kutosha kupitisha hewa
-
Iwe
na mlango wa kuingia kufanya usafi
-
Iwe
na ukubwa (nafasi) unaolingana na idadi ya kuku. Wastani wa kuku 10-15 kwa mita
moja mraba
Mambo
muhimu ndani ya nyumba
-
Chaga za kulalia kuku
-
Sakafu iwekwe maranda (wood shavings), makapi ya mpunga,
n.k
-
Viota vya kutagia mayai sentimita 35x35x35 na idadi ya
viota iwe nusu ya idadi ya kuku waliofikia hatua ya kutaga na viwekwe sehemu
iliyojificha (faragha)
UATAMIAJI WA MAYAI
Kuna
njia 2
Kumuandaa kuku anayeatamia
-
Weka
maranda au majani makavu ndani ya kiota
-
Anapokaribia kuatamia toa mayai ndani ya kiota pamoja na
maranda, hakikisha mikono haina manukato
-
Nyunyiza dawa ya kuua wadudu (viroboto, utitiri n.k) ndani
ya kiota, pia mnyunyizie dawa kuku anayetarajia kulalia mayai
-
Rudisha mayai kwenye kiota ili kuku aanze
kuatamia
-
Kwa
kawaida kuku hulalia mayai yake kwa muda wa siku 21 ndipo
huanguliwa
ULEAJI
WA VIFARANGA
Kuna
njia mbili
-
Njia
ya kubuni
-
Njia
ya asili
Njia
ya ASILI
Kuku
mwenyewe hutembea na vifaranga akivisaidia kutafuta chakula. Ni vizuri kumtenga
kuku mwenye vifaranga katika chumba chake pekee ili vifaranga wasishambuliwe na
kuku wengine hali kadhalika kuwalinda na wanyama na ndege wanaoshambulia
vifaranga.
Njia
ya KUBUNI
Vifaranga huwekwa kwa pamoja kwenye chumba maalum na
kupatiwa joto maalum, chakula pamoja na maji. Tumia taa ya kandili (chemli),
umeme au jiko la mkaa na hiyo taa iweke kwenye mzingo(mduara) walipo vifaranga.
Pia kuna kifaa kinaitwa Kinondoni Brooder ni kizuri kwa kutunzia vifaranga. Kwa
kutumia kifaa hiki kuku wanaweza kunyang'anywa vifaranga vyao mara tu baada ya
kutotoa na kuviweka kwenye hii brooder na hao kuku wakaachwa bila vifaranga
vyao, baada ya majuma matatu au manne, kuku hao huanza tena utagaji na kuendelea
na uatamiaji hadi kutotoa tena. Kwa mtindo huu kuku anaweza kutotoa mara 5-6
badala ya kama ilivyo sasa mara 2-3 kwa mwaka. Vifaranga vikae ndani ya brooder
majuma 3-4 na baadaye fungua milango ya brooder kuruhusu vifaranga vitoke na
kuzungukazunguka chumbani bila kuvitoa nje kw kipindi cha mwezi mmoja au zaidi
kutegemeana na mazingira.
KULISHA KUKU WA KIENYEJI
Kuku
mkubwa huhitaji gramu 120 za chakula kwa siku, ni vizuri kuku wanaofugwa huria
(free range) kupatiwa chakula cha ziada gramu 30 kila siku nyakati za
jioni.
Kuku
walishwe
-
Mizizi-mihogo, viazi vitamu, mbatata, magimbi,
n.k
-
Nafaka-mahindi, Mpunga, Mtama, Ulezi na Pumba za nafaka
zote
-
Mboga-Mikundekunde, nyanya, milonge, majani ya
mapapai
-
Matunda-Mapapai, maembe, n.k
-
Mbegu za Mafuta-Karanga, ufuta, mashudu ya pamba, alizeti,
n.k
-
Unga
wa dagaa
-
Maji
KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU
-
Pumba.............kilo20
-
Mashudu ya Pamba n.k...kilo 3
-
Dagaa iliyosagwa.........kilo 1
-
Unga
wa majani uliokaushwa kivulini na kusagwa........kilo 2
-
Unga
wa Mifupa ..........kilo 0.25
-
Chokaa ya mifugo ........kilo 0.25
-
Chumvi........................gramu 30
-
Vichanganyio/Premix...gramu 25
KUPANDISHA
-
Uwiano wa mitetea na jogoo ni mitetea 10-12 kwa jogoo
mmoja
-
Sifa
za mtetea ni mkubwa kiumbo, mtagaji mayai mengi, muatamiaji mzuri na mlezi wa
vifaranga
-
Sifa
za jogoo ni awe mkubwa kiumbo, miguru imara na yenye nguvu, mrefu,
upanga/kilemba kikubwa, awe na uwezo wa kuitia chakula mitetea na awe na tabia
ya kupenda vifaranga
-
Jogoo huanza kupanda akiwa na umri wa miezi 7-10 na
kuendelea hadi miaka mitatu na asipande watoto wake
-
Mitetea huanza kutaga wakiwa na miezi
6-8
MAGONJWA YA KUKU
1.
Mdondo/New castle
Virus
vinavyosababisha ugonjwa huu huenezwa kwa hewa
Dalili
-
Kuhalisha choo cha kijani na njano
-
Kukohoa na kupumua kwa shida
-
Kupinda shingo kwa nyuma
-
Kuficha kichwa katikati ya miguu
-
Kukosa hamu ya kula na kunywa
-
Idadi kubwa ya vifo hadi 90%
Kinga
-
Chanjo (New Castle vaccine) kwa mpango wa siku 3, wiki 3,
miezi 3
-
Epuka kuingiza kuku wageni
-
Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa
ugonjwa
-
Zingatia usafi wa mazingira
NDUIYA
KUKU/ FOWL POX
Virus
huambukizwa kupitia jeraha au mbu
Dalili
Kinga
-
Chanja vifaranga wanapofikia mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo
ya Fowl pox vaccine
-
Epuka kuingiza kuku wageni
-
Zingatia usafi wa mazingira
HOMA
YA MATUMBO/FOWL TYPHOID
-
Kuharisha kinyesi cha kijani na nyeupe
-
Kuku
hukosa hamu ya kula
-
Kuku
hukonda
-
Vifo
hutokea kidogo kidogo kwa muda mrefu
-
Kinyeshi hushikamana na manyoya
Tiba
Dawa
aina ya antibiotic, sulfa na vitamini
Kinga
MAFUA
YA KUKU/INFECTIOUS CORYZA
Hutokana na bakitelia na hushambulia hasa kuku
wakubwa
Dalili
-
Kuvimba uso
-
Kamasizilizochanganyikana na usaha unaonuka
-
Macho huvimba na kutoa machozi na pengine
upofu
-
Hukosa hamu ya kula
-
Mbawa huchafuka na kutoa harufu
mbaya
Tiba
Dawa
za Antibiotic, sulfa na vitamini
KUHALISHA DAMU/COCCIDIOSIS
Husababishwa na vijidudu vya Protozoa
Dalili
MINYOO
Dalili
-
Kunya minyoo
-
Hukosa hamu ya kula
-
Hukonda au kudumaa
-
Wakati mwingine hukohoa
Tiba
Dawa
ya minyoo/Pipeazine citrate kila baada ya miezi mitatu
WADUDU
Viroboto, chawa, utitiri
Dalili
Kuzuia
-
Ziba
mipasuko sakafuni na kwenye kuta za banda
-
Fagia banda mara mbili kwa wiki
-
Nyunyiza majivu au chokaa mara moja kwa wiki mara baada ya
kufagia
-
Choma masalia ya mayai yaliyoanguliwa
-
Nyunyiza dawa kwenye viota
-
Weka
maranda, majani makavu, makapi ya mpunga ya kutosha sakafuni ndani ya banda la
kuku
-
Fuata kanuni za chanjo
-
Tenga kuku wagonjwa wakae mbali na kuku
wazima
UPUNGUFU WA VIINI LISHE KWENYE CHAKULA
Dalili
-
Kuku
hupungua damu, uzito na kudumaa
-
Mifupa huwa laini na kutokuwa imara
-
Hutaga mayai yenye gamba laini na madogo
-
Huwa
na manyoya dhaifu
KAZI KWENU WAFUGAJI...!!!!!!